Siku ya Jumapili ya tarehe 13 Aprili 2014 muda
wa saa 4.20 Asubuhi, Wageni waliwasili Uwanja wa Ndege Mjini Sumbawanga kwa
kutumia usafiri wa Ndege inayomilikiwa na Kampuni ya AOURIK AIR, wakitokea Jiji
la Dra es salaam. Walipokelewa na viongozi wa JUMARU Mkoa wa Rukwa wakiongozwa
na Mwenyekiti JUMARU Mkoa wa Rukwa Mzee Ernerest Mpendakazi Kinunda na Katibu
Msaidizi JUMARU Taifa Bwana Ardius James Kwimba.
Mara
baada ya wageni kupokelewa viongozi wa
JUMARU walichukua furusa ya kusalimiana nao,kutambulishana na kuwakaribisha
katika Mji wa Sumbwanga,. Kisha walianza Msafara kuelekea Kanisa kuu la
Cathedral kwa Baba Askofu Damiano Kyaruzi Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga,
kwa ajili ya kwenda kuripoti na
kumjulisha ujio wao. Walipofika kwa Baba Askofu hawakuweza kubahatika kuonana
naye kwa kuwa alikuwa safarini na viongozi wote wa Jimbo(Mapadri) walikuwa
kwenye Ibada ya Dominika ya Matawi,hivyo Mwenyekiti JUMARU Mkoa alifanya
mawasiliano na Padri Demisius Kazonde kwa njia ya simu na kutoa idhini ya
kuwapeleka wageni/watalaamu katika majengo ya Katandala Misheni. Walipofika
katika majengo ya Katandala Misheni walianza kukagu,kupima na tathimini
waliongozwa na Mtalaam wao wa Ujenzi Engineer Osca Ferrao waliyetoka naye Jiji
la Dar es salaam pamoja na Vijana wawili wakazi wa Mjini Sumbawanga ambao
Mwenyekiti JUMARU Mkoa wa Rukwa aliwaomba kuwasaidia watalaamu kupima majemgo
hayo.
Ilipofika
muda wa 8:15 mchana walisitisha zoezi la upimaji kwa muda iliwakapate
chakula. Viongozi wa JUMARU waliwapeleka wageni kula chakula katika Hotel ya
Mbizi Forest mahali palipo andaliwa Maalumu kwa Ugeni huo rasmi. Mara baada ya
kula chakula, wageni pamoja na viongozi wa JUMARU walianza Msafala kuelekea
eneo la Malangali kuona ardhi –mahali pa kujengea Chuo Kikuu, walipofika katika
eneo hilo la Malangali waliangalia na kufanya tathimini ya kuwa panafaa
kutumika kujengea Chuo Kikuu. Aidha Mwenyekiti JUMARU alikuwa akiendelea na
utaratibu wa kufanya mawasilano na mawakala wa Makapuni ya Ndege ili kuwafanyia
wageni “Booking” ya tiketi za usafiri wa
Ndege kuanzia Mbeya hadi Dar es salaamu kwa kesho yake siku ya tarehe 14 April
2014 jambo ambalo alilikamisha kwa
wakati na ufanisi mkubwa kwani wageni kupata uhakika wa safiri yao ya kurudi
Dar es salaam mapema . Baada ya kuangalia ardhi ya Malangali walianza msafala
wa kurudi katika eneo la majengo ya Katandala Misheni kuendelea na Upimaji pamoja
tathimini namna ya kufanya ukarabati, kazi ambayo ilichukua masaa mengi hadi
kufika saa 1: 45 jioni.
Baada
ya kufanya kazi ya Upimaji na Tathimini, mnamo saa 2:15 usiku mwenyekiti JUMARU
Mkoa aliitisha kikao cha Mazungumuzo Mafupi na Watalaamu wa Chuo Kikuu cha
St.Joseph. Katika mazungumuzo waliahidi kufanya ukarabati mapema ili chuo Kikuu
kianze Mwezi wa Septemba-Oktoba 2014, walifafanua kuwa baada ya kurudi Dar es
salaam watawasilisha taarifa yao ya upimaji na thathimini ya Gharama za
kukarabati Majengo ya Katandala kwenye Bodi ya Chuo Kikuu cha St.Joseph Dar es
salaam ili kuidhinisha kutoa fedha za kuja kutumia kukarabaati Majengo ya
kuanzishia Chuo Kikuu eneo la Kandala Misheni Mjini Sumbawanga. Watalaamu wa
Chuo Kikuu cha St.Joseph waliahidi wataandaa ripoti ya namna ya kukarabati
pamoja na gharama zake na kuiwasilisha/kuituma kwa Baba Askofu Jimbo Katoliki
Sumbawanga na JUMARU itatumiwa nakala ya ripoti hiyo. Pia waliahidi kuja
kufanya uhamasishaji na Matangaozo ya Chuo Kikuu mara baada ya kufanya
ukarabati, kwa wadau wa elimu hasa walimu pamoja na Wanafunzi Shule za Msingi
na Sekondari kuhusu usomaji na ufundishaji wa Masomo ya Sayansi na programu za
Komputa ndani ya Mkoa wa Rukwa, ili kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi na
kupata fursa ya kusoma kozi za Sayansi katika Chuo cha St.Joseph Mjini
Sumbawanga. Jambo ambalo litatia chachu ya Maendeleo ya Mkoa wa Rukwa na nchi
yetu ya Tanzania kwa kupata Watalaamu wengi katika tasinia ya Sayansi na
Teknolojia. Katibu Msaidizi JUMARU Taifa, kwa niaba ya Viongozi na wajumbe wa
JUMARU aliwashukuru sana watalaamu wa Chuo Kikuu cha St.Joseph kwa kuitikia
wito wa kuja kufanya kazi ya upimaji na thathimini ya majengo kwa ajili ya
kuanzishia Tawi la Chuo Kikuu cha St.Joseph Mjini Sumbawanga, na aliwaahidi kuwa
JUMARU itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha St.Joseph bega kwa bega katika ajenda za Maendelea
ndani na nje ya Mkoa wa Rukwa ili kufikia azima ya Maendeleo na Matokeo Makubwa
kwa sasa kwa Wakazi wa Mkoa wa Rukwa chini ya mwavuli wa kutumia fursa na rasilimali
zilizopo ndani na nje ya Mkoa wa Rukwa.
Aidha,
mara baada ya mazungumuzo hayo mafupi Mwenyekiti wa JUMARU Mkoa aliahirisha
kikao kwa kuwashukuru wageni/ Watalaamu wa Chuo Kikuu cha St.Joseph na
kuwatakia mapumuziko mema ya usiku,safari njema ya kesho yake pamoja na
mafanikio mema ya shughuli zao za Maendeleo.Wageni walienda kupumuzika na Viongozi wa JUMARU
walirejea nyumbani kwako kwa mapumuziko ya usiku.
Mnamo
saa 12:00 asubuhi siku ya tarhe 14 April 2014 Wageni walianza safari ya
kuelekea Mbeya kwa kutumia Gari yao waliyokuwa wameiagiza kutoka Tawi la Chuo
Kikuu cha St.Joseph mjini Songea, walipofika Mbeya walipanda Ndege kuelekea Dar
es salaam na walifika Mapema mnamo saa 8:30 mchana siku hiyo hiyo ya tarehe 14
Aprili 2014.
JUMARU:
Kwa Rukwa Endelevu Pamoja Tunaweza.
Imeandaliwa
na Sekretarieti ya JUMARU Sumbawanga
................................................................
No comments:
Post a Comment
regnard