Mnamo
siku ya Ijumaa ya tarehe 14 machi 2014 muda wa saa 8.30 mchana Professa Bernard
Kasimila Makamu Mwenyekiti wa Mchakato wa Kuanzisha Chuo Kikuu Mkoa wa Rukwa na
Balozi Titus Simsamba Katibu wa Mchakato wa Kuanzisha Chuo Kikuu Mkoa wa Rukwa,
waliwasili Kwa njia ya basi Mjini Sumbawanga kutokea Mbeya na Dra es
salaam,walipokelewa na Wajumbe wa JUMARU Mkoa wa Rukwa na kuelekea moja kwa moja
Hotel ya Mbizi Forest mahali palipo andaliwa Maalumu kwa Ugeni huo rasmi.
- KUWASILI
WAJUMBE WA JUMARU KATIKA HOTEL YA MBIZI FOREST KUPOKEA UGENI
Mnamo saa 11.30 jioni Wajumbe wa JUMARU Mkoa
wa Rukwa wakiongozwa na Mwenyekiti wa JUMARU Mkoa wa Rukwa Mzee Ernerest
Mpendakazi Kinunda pamoja na Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi Askofu wa
Jimbo Katoliki Sumbawanga aliyeambatana na Padri Demisius Kazonde Mkrugenzi wa
CARTAS Jimbo Katoliki Sumbawanga, walikusanyika katika ukumbi mdogo uliopo
Hotel ya Mbizi Forest Mjini Sumawanga ulioandaliwa na Wajumbe wa JUMARU Mkoa wa
Rukwa kwa ajili ya kupokea ugeni wa Dr. Anath na timu yake.
- TAARIFA YA SAFARI
YA DR.ANATH
Mara
baada ya wajumbe wa JUMARU kuwasili katika ukumbi huo wa Hotel ya Mbizi Forest,
Katibu Msaidizi JUMARU Taifa Bwana Ardius James Kwimba aliwapatia wajumbe
taarifa juu ya maendeleo ya Safari ya Dr.Anath na timu yake,kuwa safari ya
Ugeni waliyokuwa wanausubiria kwa hamu ni nzuri kwani wageni wanakaribia kufika
Sumbawanga Mjini, hii ini kutokana na namna alivyokuwa anafanya Mawasiliano na
Dr. Anath akiwa safarini. Wajumbe wa JUMARU pamoja na Mhashamu Baba Askofu
Damian Kyaruzi walifurahi sana kupata taarifa juu maendeleo ya wageni waliokuwa
wakisubiriwa kupokelewa.
Aidha
Katibu Msaidizi JUMARU Taifa Bwana Ardius James Kwimba, aliendelea kufanya
mawasiliano ya mara kwa mara na Dr. Anath akiwa Safarini kuja Sumbawanga.Huku
Wajumbe wa JUMARU pamoja na Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi Askofu wa Jimbo
Katoliki Sumbawanga na Padri Demisius Kazonde, wakiendelea na mazungumuzo ya
kubadilishana mawazo kuhusu Maendeleo ya Mkoa wa Rukwa na Changamoto
zinazoukabili Mkoa na namna ya Kukabiliana
nazo.
Mnamo
saa 3:00 usiku Katibu Msaidizi JUMARU Taifa Bwana Ardius James Kwimba, alifanya
mawasiliano na Dr. Anath juu ya hali ya safari, na akamweleza kuwa kuna mvua
kubwa inanyesha kwa hiyo Dreva anaendesha Gari taratibu. Dr. Anath alitoa ujumbe
kupitia kwa Bwana Kwimba kuwa anaomba Baba Askofu na Wajumbe wengine waende
wakapumuzike kwa kuwa imekuwa usiku na yeye na timu yake bado wako njiani kuja
Sumbawanga Mjini, aliwaomba aonane nao
kesho yake Asubuhi. Katibu Msaidizi JUMARU Taifa Bwana Kwimba
aliwajulisha wajumbe kupitia ridhaa ya Mwenyekiti JUMARU Mkoa wa Rukwa.
- MAZUNGUMUZO
MAFUPI YA WAJUMBE
Baada
ya ujumbe huo kutoka kwa Dr.Anath, Mwenyekiti wa JUMARU Mkoa wa Rukwa Mzee
Ernerest Mpendakazi Kinunda alifungua kikao cha Mazungumzo mafupi ya Wajumbe wa
Jumaru pamoja na Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi Askofu wa Jimbo Katoliki
Sumbawanga na Padri Demisius Kazonde Mkrugenzi wa CARTAS Jimbo Katoliki
Sumbawanga akiwepo Professa Bernard Kasimila Makamu Mwenyekiti wa Mchakato wa
Kuanzisha Chuo Kikuu Mkoa wa Rukwa na Balozi Titus Simsamba Katibu wa Mchakato wa
Kuanzisha Chuo Kikuu Mkoa wa Rukwa. Mwenyekiti wa JUMARU Mkoa wa Rukwa
aliwapitisha wajumbe wa kikao hicho kwenye ratiba ya Ujio wa ugeni wa Dr. Anath
iliyokuwa imeandaliwa na Wajumbe wa Sekretarieti JUMARU Sumbawanga.
Aidha
wajumbe wa kikao walianza kutoa ushauri juu ya kwenda na ratiba ya ujio wa
Ugeni. Kisha Mwenyekiti wa JUMARU Mkoa wa Rukwa aliitimisha kwa kumshukuru Baba
Askofu Damian Kyaruzi na Padri Demisius Kazonde pamoja na Wajumbe wa JUMARU
Mkoa wa Rukwa kwa kuitikia wito wa kuja kuupokea Ugeni wa Dr.Anath. Mwenyekiti
walimruhusu Baba Askofu Damian Kyaruzi na Padri Demisius Kazonde pamoja na
wajumbe wa JUMARU waende wakapumuzike kwa kuwa imekuwa usiku wageni wetu
tutaonana nao kesho asubuhi kadri ya ratiba ilivyopangwa.Baada ya wajumbe
kutawanyika Mwenyekiti wa JUMARU Mkoa wa Rukwa, aliteuwa wajumbe waliobaki kuumpokea Ugeni wa Dr.Anath, wajumbe
hao ni Gaudence Mwanandenje, Chasuka,Ardius James Kwimba na Mwenyekiti JUMARU
Mkoa.
- KUWASILI WAGENI
Mnamo
saa 4:15 usiku Dr.Anath na timu yake waliwasili Hotel ya Mbizi Forest na
kupokelewa na wajumbe waliokuwa wameteuliwa wakiongonzwa na Mwenyekiti JUMARU
Mkoa.Baada ya wageni kupokelewa walionyeshwa vyumba vyao vya kulala kisha
kuonyeshwa ratiba iliyokuwa imeandaliwa.Muda wa saa 4.45 Wajumbe walioteuliwa
kuupokea Ugeni walianza kurejea nyumbani kwao kupumzika kwa kutumia usafiri wa
gari ya Mwenyekiti JUMARU Mkoa wa Rukwa.
- KUANZA MSAFALA
Asubuhi
saa 2.30 siku ya Jumamosi ya Tarehe 15 Machi 2014,Wageni na baadhi ya wajumbe
wa JUMARU mkoa walianza msafala kwenda Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ajili
ya kuripoti na kusaini katika kitabu cha wageni. Bahati mbaya Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa ilikuwa imefungwa kwa kuwa watumishi walienda Mtowisa kuhudhuria
Maadhimisho ya Utepe Mweupe uliofanyika Kitaifa katika Kijiji cha Mtowisa.Hivyo
msafala wa Dr. Anath na wajumbe wa JUMARU walienda kuripoti na kusaini kitabu
cha wageni katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga, ambapo
walimkuta Afisa Elimu Taaluma Sekondari Bwana Komba aliye achiwa ofisi na
maagizo ya kushiriki katika ugeni wa Dr.Anath.Baada ya kusaini kitabu cha
wageni ofisi ya Mkurugenzi Manispaa Msafala wa DR.Anath ulielekea Ofisini kwa
Mhashamu Baba Askofu Damian Kyaruzi Askofu wa Jimbo Katoliki sumbawanga kwa
ajili ya kwenda kusalimiana na kufanya Mazungumzo naye juu ya Ugeni na Mchakato
wa kuanzisha Tawi la Chuo Kikuu cha
St.Joseph katika Majengo ya Katandala Misheniy aliyotolewa na Baba Askofu
Damian Kyaruzi Askofu wa Jimbo Katoliki sumbawanga.
- KUWASILI OFISINI
KWA BABA ASKOFU JIMBO KATOLIKI SUMBAWANGA
Mnamo
saa 3:00 asubuhi siku hiyo ya tarehe15 Machi 2014,Msafala wa Dr.Anath na
Wajumbe wa JUMARU ulifika Ofisini kwa
Baba askofu Jimbo Katoliki Sumbawanga na kupokelewa na Baba Askofu Damian
Kyaruzi Askofu wa Jimbo Katoliki sumbawanga na mapadri wasaidizi wake. Baba
Askofu alifurahi sana kuona Msafara wa Ugeni wa Dr. Anath na Wajumbe wa JUMARU.
Mara baada ya kusalimiana naye na kusaini katika kitabu cha wageni alianza kwa
kuwakaribisha Dr.Anath na timu yake na kisha wajumbe wa JUMARU akiwepo Professa
Kasimila na Balozi Titus Simsamba.
- MAELEZO YA
VIONGOZI WA JUMARU NA MCHAKATO WA CHUO KIKUU
Mazungumzo
yalianza kwa utambulisho kwa Wageni wote alioambatana na Dr.Anath pamoja na
Wajumbe wa JUMARU.Aidha Mwenyekiti JUMARU Mkoa alimkaribisha Professa Kasimila
Kutoa Historia fupi ya Mchakato wa Kuanzisha Chuo Kikuu ndani ya Mkoa wa Rukwa
na namna JUMARU ilivyounganisha nguvu za pamoja za wanarukwa na Wadau wa
Maendeleo Mkoa wa Rukwa kushirikiana na
Dr. Anath kuanzisha tawi la Chuo cha St.Joseph Mkoa wa Rukwa kwa kuanzia katika
Majengo ya Katandala Misheni yaliyotolewa na Baba Askofu Damian Kyaruzi Askofu
wa Jimbo Katoliki sumbawanga. Pia Professa Kasimila alitoa Ujumbe kutoka kwa
Kadinari Pengo kuwa anasubilia kwa hamu Chuo Kikuu kuanza ndani ya Mkoa wa
Rukwa na ndiyo itakuwa furaha yake kuu.
- MAELEZO YA DR.ANATH
Baada
ya Professa Kasimila Kutoa Historia fupi ya Mchakato wa Kuanzisha Chuo Kikuu
ndani ya Mkoa wa Rukwa, Dr.Anath alianza Kuelezea juu ya Matawi mbalimbali ya
Chuo cha St. Joseph katika Afrika na
Tanzania. Aidha alitoa ufafanuzi kwa kina kuwa Chuo KiKuu cha St.Joseph na
Matawi yake kinamilikiwa na Shirika la Masisista lililoko India Chini ya Kanisa
Katoliki na hapa Tanzania Shirika hilo lipo.Dr.Anath aliendelea kutoa Muundo wa
Uongozi uliopo katika Chuo Kikuu cha St. Joseph pamoja na Matawi yake, kuwa
kuna Mkurugenzi ambaye huwa anafanya kazi chini ya Baba Askofu wa Jimbo
Katoliki mahali ambako Tawi la Chuo Kikuu lilipo na ripoti ikiandaliwa huwa
lazima ipitie kwa Baba Askofu wa Jimbo Katoliki wa mahali Chuo kilipo.
Dr.
Anath aliendelea kusema kuwa Amefurahi sana kukutana na Viongozi wa JUMARU
waliomuunganisha kwa Kadinari Pengo,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania pamoja na Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga.Aliahidi kuwa
atawatuma Wataalamu wa Chuo cha St.Joseph walioko Dar es salaam waje wafanye
ukarabati katika majengo yakuanzia yaliyopo Katandala Misheni, ndani ya miezi
sita na Chou kianze mwenzi Oktoba 2014. Katika kuanzisha Tawi la Chuo Dr. Anath
alisema watatoa mwelekeo wa chuo kwa kuangalia Mahitaji ya Mkoa wa Rukwa, aina ya
wanafunzi na hasa katika vipaumbele vya
kozi za Sayansi na kozi ambazo zitakidhi Mahitaji ya Mkoa wa Rukwa na watu
wake.
- MAELEZO YA BABA
ASKOFU
Mhashamu
Baba Askofu Damian Kyaruzi Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga, aliwakaribisha
na kuwashukuru wageni wote pamoja na Viongozi wa JUMARU kumuunganisha na
Dr.Anath kwa Maendeleo endelevu ya Mkoa wa Rukwa. pia alianza kutoa hitoria ya
Maendeleo ya Jimbo la Sumbawanga ambayo inajumuisha Mkoa wa Rukwa Pamoja na
Mkoa Mpya wa Katavi (kabla haija gawanywa),Baba Askofu alitoa Changamoto
mbalimbali zilizo athiri Maendeleo ya Jimbo ukiwemo Mfumo wa Ukoloni na Mifumo
ya Kisiasa, ambazo zimepelekea rasilima za Jimbo kutotumika vizuri kwa Maendeleo ya Mkoa
wa Rukwa na Katavi. Aidha Baba Askofu alifafanua kwa kina juu ya Maendeleo ya
Elimu Mkoa wa Rukwa kuwa yako nyuma ukilinganisha na Mikoa mingine kama Mkoa wa
Dar es salaam, Kagera, Mbeya na Mikoa Mingine kuanzia shule za Msingi,
Sekondari,Shule za Kidato cha tano na Vyuo mbalimbali na kwa sasa kuna Chuo
Kikuu kimoja tu ambacho ni Chuo Kikuu Huria . Pia Baba Askofu alitoa ufafanuzi
jinsi Viongozi wa JUMARU walivyo Mshirikisha juu ya Mchakato wa Chuo kikuu
ndani ya Mkoa wa Rukwa pamoja na Ujio wa Dr.Anath, alisema leo kumuona Dr.Anath
amepata majibu na Matumaini juu ya kuanzisha Chuo Kikuu ndani ya Mkoa wa Rukwa.
Baba
Askofu alitoa ujumbe kwa Viongozi wa JUMARU
na Wadau wa Maendeleo Mkoa wa Rukwa, kwa sasa kila mtu ataitazama JUMARU
kuwa chombo cha Kuwaunganisha watu kwa Maendeleo. Alitoa wito kwa JUMARU
kuendelea na mikakati ya kutoa elimu kwa
wanafunzi kupenda kusoma Masomo ya Sayansi ili wapate fursa ya kusoma chuo na
Mkoa kupata wataalamu wakutosha kwa Maendeleo ya Mkoa wa Rukwa na Tanzania kwa
ujumla. Aidha Baba Askofu alitoa ruhusa ya Majengo ya Katandala Walei yatumike
kuanzisha Tawi la St.Joseph Mjini Sumbawanga, na aliruhusu Msafala wa Dr.Anath
na Wajumbe wa JUMARU wakiongozwa na Padri Kazonde kwenda kutembelea Majengo ya
Katandala Walei.
- NENO LA
SHUKURANI
Mjumbe
wa JUMARU Mkoa wa Rukwa Mzee Nkoswe kwaniaba ya wajumbe wa JUMARU, alitoa
shukurani kwa Baba Askofu kuitikia wito wa kuupokea Ugeni wa Dr.Anath pamoja na
wajumbe wa JUMARU,ikiwemo wito wa kuruhusu Majengo ya Katandala kutumika
kuanzisha Chuo Kikuu Mjini Sumbawanga. Aidha Mzee Nkoswe aliwashukuru wageni
wote waliombatana na Dr.Anath kuitikia wito wa JUMARU kuja Sumbawanga kuanzisha
Tawi la Chuo Kikuu cha St.Joseph. Baada ya neno la shukurani wajumbe walipata
Baraka ya Baba Askofu na kisha kuendelea na msafala wa kwenda kuangalia Majengo
ya kuanzia Chuo Kikuu yaliyopo Katandala Walei.
- KUTEMBELEA
MAJENGO YA KATANDALA WALEI
Msafala
wa Dr.Anath na Wajumbe wa JUMARU
wakiongozwa na Padri Kazonde walifika eneo la Katandala na Kuangalia Majengo ya
Kumbi za Walei kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu Mjini Sumbawanga.Dr. Anath na
wajumbe alioambatana nao walifurahi sana kuona Majengo ya Katandala Misheni
Kumbi za Walei, na kutoa maoni yao kuwa Majengo yanafaa sana kuanzisha Chuo
kikuu kwani yamepangiliwa vizuri na yanatosha kuanzia isipokuwa yatafanyiwa
ukarabati ndani ya miezi sita na chuo Kikuu kianze mwezi wa Oktoba mwaka
2014.Aidha Dr.Anath alitoa agizo kwa Wajumbe wa JUMARU kuchora ramani ya
Majengo ya Katandala na Kumtumia ili akawasilishe kwenye Kikao cha Bodi ya Chuo
Kikuu cha St.Joseph Dar es salaam. Baada ya kuangalia Majengo ya Katandala
Misheni Msafala ulielekea eneo la Malangali kwenda kuangalia ekari 40 sehemu
ambapo Chuo Kikuu kinaweza kujengwa.
- KUTEMBELEA ENEO
LA MALANGALI
Msafala
wa Dr.Anath na Wajumbe wa JUMARU ulifika eneo la Malangali na kuridhika na eneo
hilo kuwa linafaa kujengwa Chuo Kikuu kwa Kuwa lipo karibu na Mjini na Huduma
za jamii kama Maji,Umeme na nyinginezo nirahisi kuzipeleka katika eneo hilo la
Malangali.Aidha Dr. Anath alitoa agizo kwa Wajumbe wa JUMARU kuwa waone
uwezekano wa upatikanaji wa Maji na Umeme kwa kuwaona wataalamu husika kama
SUWASA,Manispaa na TANESCO Mkoa wa Rukwa. Baada ya kutembelea kuangalia eneo la
Malangali Msafala ulielekea kwenda Kuona Eneo la Pito.
- KUTEMBELEA ENEO
LA PITO
Msafala
wa Dr.Anath na Wajumbe wa JUMARU ulifika eneo ya Pito kuangalia sehemu ya
Kujenga Chuo Kikuu. Dr. Anath na wajumbe aliokuwa ameambatana nao waliona eneo
hilo na kutoa maelezo kuwa eneo la Malangali linafaa zaidi kujenga chuo Kikuu. Baada
ya kuona Eneo la Pito Dr. Anath na Wataalamu alioambatana nao waliagana na
Wajumbe wa JUMARU Mkoa wa Rukwa, kisha walianza Safari ya Kuelekea Mbeya hadi
Dar es salaam. Aidha Wajumbe wa JUMARU walianza Safari ya kutoka Pito kurudi
Mjini Sumbawanga na walikubaliana kuwa mara baada ya kufika Sumbawanga Mjini
watafanya kikao saa 12.30 jioni siku ya 15/03/2014 katika Ukumbi Mdogo wa Hotel
ya Mbizi Forest, cha tathimini ya Ugeni wa Dr.Anath kutembelea Majengo ya
Katandala Misheni,Ardhi ya Malangali na Pito.
- KIKAO CHA
TATHIMINI YA UGENI WA DR.ANATH KUTEMBELEA MAJENGO YA KATANDALA,ARDHI YA
MALANGALI NA PITO.
Mnamo
saa 12.30 Wajumbe wa JUMARU Mkoa wa Rukwa walikusanyika katika Ukumbi Mdogo wa
Hotel ya Mbizi Forest. Katibu Msaidizi wa JUMARU Taifa alimkaribisha Mwenyekiti
JUMARU Mkoa wa Rukwa Mzee Ernerest Mpendakazi Kinunda kufungua kikao cha tathimini
ya Ugeni wa Dr.Anath kutembelea Majengo ya Katandala Misheni,Ardhi ya Malangali
na Pito.
Mwenyekiti
JUMARU Mkoa, alifugua kikao kwa kuwasalimia wajumbe, pia kuwakumbusha wajumbe
tuliko toka,tulipo na kiu ya kusonga mbele katika Maendeleo endelevu ya Mkoa wa Rukwa kupitia JUMARU.Kisha aliwakaribisha
Wajumbe kuchangia thathimini ya Ugeni wa Dr.Anath.
Professa
Kasimila alitoa shukurani kwa niaba ya Wajumbe wa JUMARU Dar es salaam na yeye
mwenyewe, kwa kushukuru Mapokezi ya Ugeni. Pia alitoa maoni ya tathimini kwa
kumwelezea Dr.Anath kuwa kauli za Dr.Anath zimejitokeza leo waziwazi,ukweli
ambao Baba Askofu ametoa kwa kunukuu
maneno ya Baba Askofu “Nimetoa Majengo” mwisho wa kunukuu alisema Professa
Kasimila. Kuhusu Eneo la Malangali Ekari
40 Dr.Anath alilikubali kuwa linafaa kujengwa Chuo Kikuu alisema Professa
Kasimila. Aliendelea kutoa Maagizo ya Msingi ya Dr.Anath kuwa ameagiza tuchore
ramani itakayo onyesha Majengo ya
Katandala Misheni,pamoja na kuonyesha upatikanaji wa Maji na namna ya kupata
Umeme katika eneo la Malangali la kujenga Chuo Kikuu. Dr. Anath amependa
Malangali kuliko Pito kwa kuwa Malangali ipo karibu na Mjini pia Majengo ya
Katandala Misheni Walei ameyakubali na hili limetujengea Imani kubwa kwa Ugeni
wa Dr.Anath alifafanua Professa Kasimila . Pia Professa Kasimila alitoa Maoni
ya Dr.Anath kuwa aliahidi Chuo Kikuu
kufundisha Kozi zinazoweza kuleta Manufaa ndani ya Mkoa wa Rukwa.
Balozi
Titus Simsamba alitoa ushauri juu ya kuhamasisha wanafunzi kusoma masomo ya
Sayansi kama Baba Askofu alivyoshauri hili liwe ndani ya Programu za JUMARU ili
Wanafunzi wapate fursa ya kusoma Chuo kikuu fani za Sayansi zitakazo leta tija
ya Maendeleo ya Mkoa wa Rukwa. Aidha Balozi Titus Simsamba waliwakumbusha
wajumbe njinsi Baba Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga alivyo watambulisha
Viongozi anaoshirikiana nao yaani Mapadri, kuwa Baba Askofu alitaka kutuonyesha
watu ambao tunaweza kushirikiana nao katika Maendeleo ya Mkoa wa Rukwa.
Wajumbe
wengine walichangia juu ya kupanga
mipango na mikakati ya kuhamshisha
wanafunzi wasome kwa bidii hasa Masomo ya Sayansi. Ikiwemo JUMARU kupanga
programu za kuhamasisha wanafunzi kuanzia ngazi ya Shule za Msingi hadi Vyuo
vyilivyopo ndani ya Mkoa wa Rukwa,kufanya Maonyesho pamoja na Mashindano kwa
wanafunzi,wananchi ndani ya Mkoa na nje ya Mkoa ili kutia hamasa kwa Wadau.
Mnamo
saa 2:45 usiku Mwenyekiti wa JUMARU Mkoa wa Rukwa aliahirisha Kikao kwa
kuwashukuru wajumbe kushiriki katika Ugeni wa Dr.Anath pamoja na kuhudhuria na
kushiriki kikao cha tathimini,kisha Wajumbe walitawanyika kwenda kupumzika.
JUMARU: Kwa Rukwa Endelevu Pamoja Tunaweza.
Imeandaliwa
na Sekretarieti JUMARU Sumbawanga
.................................................
No comments:
Post a Comment
regnard