JUKWAA
LA MAENDELEO MKOA WA RUKWA
S.L.P. 666
SUMBAWANGA.
30/12/2013
Kumb.NA:JUMARU/RK/AD.6/RUU/VOL.I/59
Mheshimiwa Mhashamu Baba Askofu
Damiani Kyaruzi
JIMBO KATOLIKI SUMBAWANGA.
TUMSIFU YESU
KRISTU!
YAH: MAOMBI YA KUKODISHIWA KWA MUDA MAJENGO YA
KANISA ENEO LA
KATANDALA (TRADE SCHOOL NA
WALEI) KWA AJILI YA KUANZISHA CHUO KIKUU – ST. JOSEPH UNIVERSITY (T) CHA WADAU
WETU.
Mheshimiwa
Baba Askofu, husika na
kichwa cha barua kilichotajwa hapo juu.
Kwa
heshima kubwa, sisi Jumuia ya wanarukwa chini ya chombo chetu tulichokianzisha
na kukisajili (Jukwaa la maendeleo mkoa
wa Rukwa (JUMARU) mahsusi kwa ajili ya kutuunganisha wanarukwa wa ndani ya
mkoa, nje ya mkoa na nje ya nchi katika kuunganisha nguvu zetu za hali na mali
ili tuweze kuhamasisha na kuchangia katika jitihada za kuleta maendeleo ndani
ya mkoa na wanarukwa kwa ujumla, tunakuomba utusaidie kutukodishia kwa muda majengo yako katika eneo la Katandala
kwa ajili ya kuanzishia Chuo Kikuu kupitia wadau ambao tumewashawishi – yaani ST. Joseph University in Tanzania.
Mradi utakuwa tayari kukarabati majengo na kufanya maboresho ili yakidhi hadhi stahiki kwa huduma husika.
ST. Joseph University in
Tanzania kupitia Dkt. Anath
kwa mazungumzo maalumu na makubaliano yaliyofanyika kati yake na kamati ya
JUMARU inayoratibu Mchakato wa kuanzisha Vyuo Vikuu ndani ya Mkoa pamoja na
Rukwa Univerisity inayoongozwa na Prof.
Athanas S. Kauzeni na Prof. Bernard J. Kasimila, alikubali ombi letu la
kujenga chuo kikuu ndani ya mkoa wetu ili nasi tupate uzoefu wa kuanzisha cha
kwetu (Affiliation of Rukwa University).
Aidha
Dkt. Anath aliomba atafutiwe majengo
ya kukodi kwa kuanzia na yupo tayari kuyakarabati na pia JUMARU imtafutie eneo
la kuanzia Ekari 40 na kuendelea kwa ajili ya kujenga majengo ya kudumu. Ardhi tayari tumepata sehemu mbili ndani ya
Manispaa ya Sumbawanga (Malangali – zaidi ya Ekari 50 na Pito-zaidi ya Ekari
100).
Hivyo basi tunaomba utusaidie
majengo ya kuanzia kwa muda pamoja na kumpokea/kuwapokea wadau wetu hawa ndani
ya Jimbo lako maana taasisi yao ipo chini ya shirika la Kanisa letu.
Jukumu kubwa la JUMARU ni
kushawishi na kuunganisha wadau wa ndani na nje ya mkoa kuwekeza ndani ya
mkoa. JUMARU ipo tayari kwa kutumia
wataalumu wake kusaidia kuhamasisha na kushauri kuwezesha wadau kufanikisha
kuwekeza miradi yao yenye tija ndani ya mkoa ambapo hata kanisa letu Jimbo kama
lina mpango wa kuanzisha Chuo Kikuu na miradi mingine ya maendeleo tupo tayari
kusaidia kwa hatua zote kufanikisha (kuhamasisha na
kushauri).
Ni
mategemeo yetu kuwa ombi letu
litapokelewa na kukubaliwa ndani ya muda huu muafaka maana kamati yetu na Dkt.
Anath wanatarajia kufika Sumbawanga kabla ya mwisho wa mwezi Januari 2014 kama tutawathibitishia kuwa majengo yamepatikana.
Majibu ya barua hii yatasaidia kumshawishi Dkt. Anath kufika Sumbawanga.
Tunatanguliza
shukrani za dhati.
Wako,
JOACHIM BENEDICT ANATORY
SIKULUMBWE
KATIBU MKUU
JUMARU – TAIFA
Nakala:
1.
Bibi
Helena Khamsini
Mwenyekiti wa JUMARU TAIFA – Aione
jaladani
2.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa
3.
Prof.
Athanas S. Kauzeni
Mwenyekiti – Kamati ya Mchakato wa Chuo
Kikuu Rukwa
UDSM – DAR ES SALAAM.
4.
Baraza
la Wazee/Wadhamini wa JUMARU
SUMBAWANGA/DAR ES SALAAM.
NB: Nimekuambatanishia
baadhi ya nakala za nyaraka na taarifa za
JUMARU.
No comments:
Post a Comment
regnard