Tuesday, 1 October 2013

Habari Kutoka Makao Makuu ya Jumaru

Ni jambo la kila mmoja wetu kumshukuru Mungu kwa Kuwajalia wanasekretariati wa Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa Rukwa JUMARU kwa kudhudhulia mwaliko maalumu wa  Mkutano mkuu wa Mkoa wa Rukwa unaojulikana kama Regional Consultative Committee (RCC) au Bunge la Mkoa. Mkutano huo ulifanyika katika mji mdogo wa laela ukiongozwa na Mkuu wa Mkoa kama Mwenyekiti ,Wabunge Wote ,Wakuu wa Wilaya ,Wakurugenzi wote ,Madiwani na wengineo wengi bila kusahau waandishi wa habari wa Mkoa.
Wajumbe wa RCC  
Wajumbe waSekretariati ya JUMARU waliongozwa na Prof. B kasilimila aliewasilisha mada ya Chuo kikuu cha Rukwa (RUU), kutoka DSM na Mjuumbe wa Jumaru Tawi la Mbeya BW, Nsokolo Kaniki (Mtaalamu wa kuongeza thamani ya mazao ) akiwasilisha mada ya Changamoto zinazo ukabili Mkoa wa Rukwa na jinsi Jukwaa hili litakavyo kabiliana nazo ikiwa moja ya majukumu katika Jukwaa hili.Kikao hiki kilitoa ushirikiano wa dhati kabisa pale mada za wajumbe zilipokuwa zinawasilishwa, wengi wametoa mchango wao wa dhati wa mawazo na Jukwaa limechukua kama changamoto za kukabiliana nazo, hasa katia Elimu ambalo limekua janga tishio la Wanarukwa.

Prof.Benard kasimila (kushoto) wa kijiji cha Chala  akiwasilisha Mada ya Rukwa university Kwa kutoa ufafanuzi kwa njia ya vitendo
Pia wajumbe hawa walitembelea Radio Chemchem (radio ya Mkoa ), kuwa tangazia wanarukwa wote wadau wa Maendeleo juu ya nini kilichowafanya wanarukwa kuanzisha hili Jukwaa, wakati wajumbe hao wakihojiana na Mtangazaji wa Radio hio, wadau mbalimbali wa Mkoa wa Rukwa walipiga simu nyingi sana kutaka ufafanuzi wa kina Juu ya Jukwaa , japo wengi wanadhani kuwa ni NGO kama NGos nyingine zilizoko katika Mkoa huo kumbe sio mara baada ya Katibu wa JUMARU kufafanua kuwa hii ni Platform iliyosajiliwa mambo ya ndani kwa madhumuni  ya Kuwaunganisha Pamoja wanarukwa waishio ndani ya Mkoa wa Rukwa na nje ya Mkoa (Mikoani) na nje ya nchi kujadili pamoja maendeleo ya Mkoa huo,
Wajumbe wa sekterariati ya Jumaru wakia radio Chemchem  
Bila kuchoka Wajumbe pia walimtembelea Askofu mkuu wa jimbo la Kanisa katoliki la Sumabwanga , na kuribishwa na Padri Mbegu (katika picha) ambapo walifanya mazungumzo ya pamoja juu Jukwaa hili na kazi zake ikiwa ni pamoja na kuanzisha Rukwa University (RUU), Padri huyo alishukuru na kuomba wakutane tena mara tu baada ya Askofu huyo kurudi katika safari yake,

Padri Mbegu, (kushito)na wajumbe wa Jumaru katika Mazungumzo ya pamoja juu ya Jukwaa
Mwisho kabisa Wajumbe waliongea na Wanarukwa wadau wa maendeleo bila Kusahau wanaVyuo vikuu walioko Mkoa huo katika Ukumbi wa Betrehem, ambapo wajumbe hawa waliendelea kutoa ufafanuzi na kukusanya mawazo wa wazawa na wadau wa Maendeleo Mkoa wa Rukwa , hatuna budi kuwashukuruni nyote mloshirikiana kwa pamoja kwa kuwezesha safari hii Mungu azidi kuwa bariki sana . na pamoja tuseme (Jumaru kwa Rukwa Endelevu Pamoja Tunaweza) 0757230097


No comments:

Post a Comment

regnard