Tuesday, 26 November 2013

Mapendekezo ya Wanajumaru wa kwenda katika ziara ya kumtembelea Waziri Mkuu Mh Peter Kayanza Pinda

Haabari za leo mabibi na mabwana wanarukwa na wadau wengine mlioko katika nchi hii na nje ya nchi, habari njema na ya kufurahisha na yenye motisha kwa Wanajumaru kukubaliwa kupewa fursa na kibali cha kufanya mazungumzo na Mh Pinda Waziri mkuu siku ya jana tarehe 16/11/2013.
Nia na madhumuni ya mzungumzo hayo hasa yalijikita katika malengo yafuatayo:
  • kulitambulisha JUKWAA LA MAENDELEO MKOA WA RUKWA (JUMARU) kwa Mh Waziri Mkuu, na mikakati yake.  
  • Mh Pinda kusalimia na Wazee wa JUMARU. 
  • Kumwomba Waziri Mkuu kwenda kua mshiriki na Mgeni rasmi kwenye kongamano la Wanarukwa Sumbawanga Desemba 2013 tarehe 20-22 , juu ya maendeleo ya Mkoa kijamii,Kiuchumi, Kisiasa, Kitamaduni na matumizi ya maliasili zake.
  • Wazee wa msafala kubadilishana mawazo na Mh Pinda.

No comments:

Post a Comment

regnard