Kwa ujumla ni kwamba inatakiwa kuibadilisha Rukwa kutoka
hali iliyopo kwa sasa ya kuelekea jangwa na kupanda miti kwa wingi ambayo
itawawezesha kuanza kusafirisha hata mbao kuelekea Dar na kwingineko. Na pia
kuokoa mazingira ya Rukwa kwani hakika jangwa linatuandama kule lazima tufanye
jitihada, wanarukwa wenzangu kuna aina mbalimbali ya miti ambayo tunaweza
kuipanda mkoani Rukwa, miti ya kuni ambayo hukuwa kwa muda mfupi na miti ya
mbao ambayo walau huchukua muda mrefu ili uweze kupata matured trees ambazo
ndio zinafaa kwa mbao utaona jinsi biashara hiyo ilivyo nzuri.
Expart Victor Sadala. kutoka - Mpui – Sumbawanga kwa sasa niko nchini Sierra Leone |
Tunashukuru serikali kwa kutengeza barabara sasa ni kazi kwetu kuruka kama jina lenyewe Rukwa linavyojieleza. Tumezoea kuona malori yanayosafirisha mbao kutoka Njombe na Mufindi ni wakati sasa wa kuona malori ya Mbao yakitokea mkoani Rukwa.
Karibuni Sumbawanga
Karibuni Sumbawanga
No comments:
Post a Comment
regnard