Saturday, 14 December 2013

Habari za leo !!!!!!!!!! Yaposuta

Ndugu Wanarukwa Seketretariati ya Jukwaa la Maendeleo Mkoa wa Rukwa (JUMARU)  inazidi kuwakumbusha Wanarukwa  na wadau wengine wapenda Maendelo ya Mkoa wa Rukwa kuwa  Kongamano litakuwa tarehe 20-22 desemba 2013 katika ukumbi wa St. Maurus chemchem (Kristu Mfalme )Sumbawanga Mjini kwa muda wa siku tatu mfululizo kwa mada za kujadili Ardhi, Elimu ,Afya, uchumi na Maliasili na Rasilimali  za Mkoa wa Rukwa kwa Maendeleo ya Wananchi. Mgeni Rasimi atakuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh Pinda (Mb) katika picha kulia 
Waziri Mkuu Mh Peter Kayanza Pinda (Mb) kulia 
Aidha Waziri Mkuu ameliahidi
Jukwaa hili kuwa atakuwepo kwa Muda wa siku tatu ,Kongamano hili litahudhuliwa na jopu la kamati lilioandaliwa la Maprofesa na Madaktari mabalimbali wazawa wa Mkoa Warukwa kama walivoainishwa katika ratiba kwaajili ya kuwasilisha mchakato wa kuanzisha Chuo Kikuu cha mkoa wa Rukwa  (RUKWA UNIVERSITY -RUU). kwa ajili ya kuboresha elimu ngazi zote kupunguza umasikini wa ujinga (Elimu).
      Wageni waalikwa ni Walimu Wakuu wote shule za msingi ,sekondari,Wakufunzi waVyuo wa mkoa ,wenyeviti wa vijiji wote na wajumbe wawili yaani mkulima na mfugaji mmoja , watendaji wa vijiji,watendaji wa kata , Waratibu elimu kata,Madiwani wote , Makatibu Tarafa ,Paroko wote na  Dini zote, NGOs zote,Wakuu wa Vyama.

upatapo tangazo hili mjulishe Mwanrukwa juu yatukio hili muhimu la Mkoa


                    KARIBUNI SANA NA RUKWA NG'ARA

 

No comments:

Post a Comment

regnard