Thursday, 26 December 2013

HERI YA CHRISMAS

Awali ya yote ungana na mimi na Wanarukwa wote walioko nje na ndani ya Mkoa wa Rukwa kwa mapenzi mema  ya Mungu ya kuweza kutufikisha siku ya leo, pia Tuungane kumshukuru Mungu kwa Uweza wake tumeweza kufanikisha Kongamano la wanarukwa wote lililoandaliwa na sekretariati ya Jukwaa la Maendeleo mkoa wa Rukwa (JUMARU). kongamano hilo limeenda vizuri sana na kuisha salama , likiwa limehudhuliwa na watu zaidi ya 600, wakiwepo wazee wetu wazalendo wa Mkoa wetu wa Rukwa ,Mzee Nkoswe,Mzee Chief Chinyonto,Dkt Mzindakaya , Mzee Kimiti,Mzee Mtuka ,Mzee Maufi, Mzee Yamsebo, Mzurikwao na wengine wengi wangalie katika picha
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katikati, kushoto kwake ni Mwenyekiti JUMARU Bi Helena Khamsini,Kulia kwake M/kiti msaidizi JUMARU Bi J. Michese 
kwa bahati mbaya mgeni Rasim aliye tegemewa kwa sababu zilizo nje ya uwezo  wake Mh Mizengo Pinda (Waziri Mkuu) hakuweza kuhudhuria na kuwamwagiza Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng Manyanya (MB) (katikakati),kutoka Bungeni na kumwakilisha , Ndugu Wanarukwa maazimio ya kongamano hilo ni mazuri ambayo kila Mwanarukwa na yeyote mpenda maendeleo ya Mkoa wetu  atafikishiwa kwa njia mbalimbali kila alipo . watu wengi wamejitoa kucha
ngia katika kile ambacho kilikua ni mada mojawapo ya Kongamano ya kuanzisha Chuo Kikuu Mkoa wa Rukwa ,
ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa NGO ya KAESO alitoa ofisi kwa ajili ya kuendesha shughuli za JUMARU,na ameahidi kutoa miti ya thamani ya milioni moja (1,000,000/=) kupanda kuzunguka Chuo Kikuu, pia mzee Nkoswe ametoa huduma zote za Stationary kwa ajili ya Ofisi ikiwa ni pamoja na Computers na Internet services , Familia moja imejitoa kutoa ekari 40 kwa ajili ya kuanza Chuo katika maeneo ya Pito katika picha ni  mwakilishi wa familia hio na kuthibitisha na mwenyekiti wa kijiji hicho mbele ya kongamano .

Mwakilishi wa familia iliyetoa Ardhi wa kuanza Chuo 

 Ndg Wanarukwa kwa heshima kubwa tunayokupa na unayoipa Sekretariati ya JUMARU usichoke kuipa ushirikiano wa hali na mali ikiwa ni pamoja na mchango wa hali na mali kufanikisha majukumu haya mazito. utaendelea kupata tarifa zaidi zinazoendelea ikiwa na jukumu moja  la kuandaa mpango mkakati (Strategic plan) ambao unaandaliwa na sekretariati hio.nawatakia kazi njema!!!!








No comments:

Post a Comment

regnard