Saturday, 4 January 2014

TAARIFA YA KUTOKA KAMATI TENDAJI YA JUMARU TAWI LA SUMBAWANGA

Ndugu Wanarukwa na wadau wa Mkoa wetu hasa wapenda Maendeleo KHERI YA MWAKA MPAYA, Ndugu zangu napenda kuwapa tarifa kutoka Kamati tendaji ya Jukwaa la Maendelo Mkoa wa Rukwa (JUMARU) 
katika kikao cha tarehe 18/12/20143 katika uteuzi ulofanyika na Mwenyekiti wa JUMARU taifa Bibi Helena Khamsini wa  baraza wazee wawakilishi wa Mkoa na Baadhi ya viongozi wa sekrikari ya Mkoa na kidinii walifika kijiji cha Pito kuona eneo lilitolewa na kuwashukuru wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa pia na diwani na mtendaji wa kata ya Pito na mmoja wa viti maalumu .Kamati hio haikuchoka tena kesho yake kamati ya wazee na uongoziwalifika  na kufanya mazungumzo ya pamoja na Baba Askofu Kyaruzi wa kanisa katoliki juu ya kuomba atusaidie kutukodishia kwa muda majengo kanisa  katika eneo la Katandala kwa ajili ya kuanzishia Chuo Kikuu kupitia wadau ambao JUMARU tumewashawishi – yaani ST. Joseph University in Tanzania.


Mzee Mtuka kati ya wazee waliotembelea eneo la Pito hilo linalooneka karibu na Mlima kuna  madhari mazuri sana
Wazee wa kijiji cha Pito katika Mkutano wa hadhara wa kuidhinisha eneo lililotolewa kwa ajili ya Ujenzi wa Chuo 

Mradi utakuwa tayari
kukarabati majengo na kufanya maboresho ili yakidhi hadhi stahiki kwa huduma husika.

ST. Joseph University in Tanzania kupitia Dkt. Anath kwa mazungumzo maalumu na makubaliano yaliyofanyika kati yake na kamati ya JUMARU inayoratibu Mchakato wa kuanzisha Vyuo Vikuu ndani ya Mkoa pamoja na Rukwa Univerisity inayoongozwa na Prof. Athanas S. Kauzeni na Prof. Bernard J. Kasimila, alikubali ombi letu la kujenga chuo kikuu ndani ya mkoa wetu ili nasi tupate uzoefu wa kuanzisha cha kwetu  (Affiliation of Rukwa University).,Askofu ameonesha kukubali wazo na kuahidi kutoa chumba cha kufikia dkt Anath  kwa mazungumzo ya pamoja mjini Sumbawanga katika kuliweka swala hili kiutendaji zaidi

No comments:

Post a Comment

regnard