Monday, 24 March 2014

TAARIFA YA ZIARA YA KAMATI YA RUKWA UNIVERSITY

Ndugu Watanzania wazalendo wapenda maendeleo ya taifa letu ,Habari ya kazi , naamini sisi wote ni wazima na wale wasio wazima poleni. Ndugu zangu napenda kuwarifu kuwa sekretariati ya Jukwaa la maendeleo mkoa wa Rukwa (JUMARU). wiki iliyopita  kamati ya mchakato wa uanzishaji wa Rukwa University iliandaa ziara ya kwenda Sumbawanga kutoka DSM. kamati hio iliongozwa na Prof.Kasimila makamu Mwenyekiti wa mchakato huo ambaye ndiye mmiliki wa chuo kimoja kilichopo opposite na Mzumbe University tawi la DSM .Lengo mahususi ya ziara hiyo ilikua ni kumpeleka Mkurugenzi wa Vyuo vya St Joseph nchini, Dr. Anath  ambaye kupitia JUMARU ndiye mwekezaji aliepatikana kufanya affiliation kuwezesha kupata Rukwa university. Mkurugenzi huyo Dr Anath kwa jina alipata fursa ya kutembezwa mjini Sumbawanga katika maeneo yote ambayo JUMARU imepewa na wenyeji wa Mkoa wa Rukwa, wapenda maendeleo ili kukamilisha mchatao wa chuo hicho. Maeneo hayo ni pamoja na Malangali karibu na crusher ya mawe , pito na Maeneo ya Katandala Mission ambayo Askofu alitoa majengo ya kuanzia. 
BALOZI - TITUS SIMSAMBA Katibu wa Kamati kuu ya mchakato wa uanzishwaji wa Rukwa University.
Aidha Dr. Anath alifuarahishwa sana na madhali ya Mkoa wetu wa Rukwa kuwa una hali nzuri, maeneo ni masafi, na kufurahishwa zaidi na mapokezi yaliofanyika na wakazi - Sekeretariati JUMARU pamoja na uongozi mzima wa Uaskofuni na kumwalika Prof, Kasimila kufanya presentation th 25/3/2014 makao makuu ya chuo cha St joseph DSM. Pia uongozi wa St. Joseph uliwahitaji Wanajumaru kupeleka Ramani za majengo yaliopo katandala mission. kwa ajili ya kuona ni jinsi gani wanaweza kuanza chuo miezi kadhaa ijayo.Enyi wadau napenda kuhitimisha kusema Mungu awatangulie wote wawezeshaji wa chakato huu , Mungu amtangulie Prof. Kasilimila Bernard katika Presentation yake .aksanteni kwa maelezo usikose kuwasiliana 0757230097


No comments:

Post a Comment

regnard