Sunday, 29 March 2015

HARAKATI ZA KUENEZA NA KUIMARISHA UTENDAJI KAZI WA JUMARU

Sekretariati ya JUMARU iliyoanzishwa kimkakati kwa nia ya kuleta maendeleo katika kutimiza adhima ya malengo ya JUKWAA, wameteuliwa wazee 20 wa mkoa wa Rukwa wanaounda Balaza la wazee. Baraza hilo likiwa chini ya col.Mzurikwao (katika picha chini) na mzee Kapele (pichani) .
pichani)
katikati ni mwenyekiti kushoto kwake ni msaidizi wake 
Baraza hili lilifanya kikao chake cha kwanza cha kufamiana na kufanya uchaguzi wa viongozi wake tarehe 7/3/2015 na kuazimia kukutana tarehe 28/3/2015. katika kikao cha jana kwa mujibu wa taarifa ya katibu mkuu wa JUMARU taifa kilifanyika baadhi ya maazimio yalifanyika ikiwa na pamoja na wajumbe wote kupata katiba ya JUMARU kuisoma na kuielewa vizuri na kuitamngaza taasisi hii mahala popote walipo wanarukwa , kila mjumbe kwenye kikao cha tarehe 25/4/2015 kuja na wanachama wapya 10, sekretarieti ya JUMARU kubuni mbinu za kuitangaza JUMARU kwa njia za Radio , magazeti, vipeperushi,Runinga ,midaharo,mikutano n.k . Aidha mwenyekiti alisisitiza umakini ,nidhamu, kuwahi katika vikao .Katika kikao hicho kilihudhuriwa na katibu wa JUMARU kilando, kasanga na kaengesa .msikilize katibu kilando hapa
Mara baada ya kumaliza kikao mlezi wa JUMARU alimaliza kikao kwa kutoa maneno ya Busara juu ya mienendo thabiti ya kuzingatia juu maendeleo ya taasisi hii. na kufngwa kwa sala na bibi Ntwenya .
Mzee Chief Chinyinto (mlezi wa JUMARU taifa)
 wito wangu kwa wanarukwa " naamini maendeleo ya mkoa wetu yataletwa na uzalendo wetu na si vinginevyo wakati wa kusubiri tuletewe maendeleo na serikali au nchi jilani yamepitwa na wakati ila ushilikishaji , nia na shauku ya mwamba ngoma kuvuta kwake ndio itayatufikisha tunapotaka na kukomboa jamii yetu pale tunapotalaji husani katika kuondoa adui mkubwa ujinga kwa kusaidia kuleta elimu katika mkoa wetu."
              katilumi   nawatakia jumapili njema

No comments:

Post a Comment

regnard