Jukwaa
la Maendeleo Mkoa wa Rukwa (JUMARU) ni
asasi ya kiraia tuliyoianzisha kimkakati mei 2009 na kisha kupata usajili
kisheria katika wizara ya Nambo ya Ndani ya Nchi tarehe 30/08/2013.
Lengo
kuu la JUMARU ni kuhamasisha nguvu za hali na mali za wanarukwa wa ndani na nje
ya mkoa katika kushawishi na kuchangia jitahada za kukabili changamoto za
maendeleo ya mkoa na wanarukwa kwa ujumla ili kuwezesha wanarukwa kufanya kazi
kwa bidii, kutambua na kutumia vyema fursa za maendeleo zilizopo, rasilimali na
maliasili za ndani ya mkoa katika kujiletea maendeleo na kuzihifadhi kwa ajili
ya vizazi vijavyo.
JUMARU
kama Taasisi hai ilizinduliwa rasmi tarehe 01/09/2013 Dar es salaam katika
ukumbi wa Urafiki Social Hall kwa kutambulisha wanachama hai na kusimika
viongozi wa kudumu kitaifa kwa miaka mitatu ya kikatiba ambapo uongozi uliokuwa
wa muda ulipitishwa na kuthibitishwa na kuteua uongozi wa muda wa tawi la Dar
es salaam. Siku ya uzinduzi wa JUMARU wanachama hai walikuwa wamefikia 37 na hadi
kufikia tarehe ya leo 19/10/2015 tumefungua matawi katika tarafa 12 na vijiji 5
ndani ya mkoa wa Rukwa na tuna wanachama hai kwenye mikoa 15 (Mwanza, Tabora,
Kigoma, Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Das es salaam,
Pwani, Iringa, Katavi, Dodoma na Katavi) na nje ya nchi 7 na kufanya tufikishe
wanachama hai 231 (waliojaza fomu za uanachama, kulipia michango, kupewa kadi
na vitambulisho rasmi vya uwanachama).
Aidha,
tarehe 20-22/12/2013 tulifanya kongamano la wanarukwa katika ukumbi wa St.
Maurus Chemchemi lililohudhuriwa na wadau zaidi ya 600,mgeni rasmi akiwa Waziri mkuu wa Tanzania Mh.
Mizengo Pinda (MB) aliyewakilishwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Eng. Stella
Manyanya (MB). Siku hiyo pia ilitumika kuzindua JUMARU kwa ndani ya mkoa na
kutambulisha uongozi rasmi na kisha kuteua
kamati ndogo ya kuratibu shughuli za JUMARU ndani ya mkoa kwa muda wa mwaka
mmoja ili kusaidia kufungua matawi ya kikatiba na utekelezaji wa mikakati
mingine hasa mchakato wa uanzishaji wa chuo kikuu ndani ya mkoa (kamati ya
uratibu ndani ya mkoa imemaliza muda wake February mwaka huu).
Katika
utekelezaji wa malengo/madhumuni ya JUMARU, tulijiwekea vipaumbele sita vya
awali ambavyo ni Elimu (uanzishwaji wa vyuo vikuu), ajira kwa vijana,kilimo bora na masoko (uongezaji wa thamani ya mazao ya kilimo na
mifugo – Agro processing), uwekezaji (rasilimali
na maliasiri),umasikini na ujasiriamali
(Uanzishaji wa JUMARU SACCOS,kuhamasisha mchakato wa Rukwa Community Bank) na upimaji na umilikishaji wa ardhi za
wananchi/mashamba (hati miliki za ardhi kwa wananchi na mgawanyo wa ardhi
ya kilimo na ufugaji kuepusha migogoro).
Hadi
sasa tumefanikisha kubuni mawazo na kushawishi na kuhamasisha uanzishaji wa
matawi mawili ya vyuo vikuu ndani ya
mkoa wa Rukwa (yaani St Joseph University in Tanzania-tayari
ukarabati wa majengo yao katandala Mission,baada ya JUMARU kuyaomba kwa Baba
Askofu Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga,unaendelea na tawi la Mbeya University of Science and Technology- MUST ambao serikali ya
mkoa, baada ya JUMARU kuwasilisha wazo kwenye kikao cha RCC kilichofanyika
katika mji mdogo wa Laela Septemba 29, 2013 juu ya kambi ya wakandarasi Kianda Kaengesa kutafutiwa tawi
la chuo kikuu kinachotoa mafunzo ya sayansi
na teknolojia,imewakabidhi kambi hiyo).
Kwa
mwaka 2014 tulijikita katika kuhamasisha masuala ya uwekezaji na kufanikiwa
kuandaa hafla maalumu tarehe
14/9/2015 katika ukumbi wa DSM Police Academy Kurasini ya kutangaza fursa za
uwekezaji ndani ya mkoa wa Rukwa ambapo mkuu wa mkoa wa Rukwa alikutanishwa na
wanarukwa waishio DSM na baadhi ya wadau na pia kushiriki maadhimisho ya miaka
40 ya mkoa wa Rukwa na lile kongamano la uwekezaji lililofanyika Sumbawanga
Uwanja wa Nelson Mandela (JUMARU ilifanikiwa kutengeneza vitenge , khanga na
T-shirt kupitia wadau wake wa maadhimisho ya miaka 40 ya mkoa na uwekezaji).
Kwa
mwaka huu 2015 na 2016; tunatekeleza mkakati wa kuhamasisha na kushawishi
uanzishaji wa JUMARU SACCOS miongoni mwa wanachama wa JUMARU tu ili
kukabili changamoto ya umasikini na kununua hisa kwenye vyombo vingine vya
fedha na kuwekeza zaidi,mchakato wa Rukwa community bank inayofanywa na wadu
husika, kijiji cha ajira na maendeleo
kwa vijana ndani ya mkoa (cha mfano kimkoa na kisha katika kila
Halmashauri kiwepo kijiji cha vijana ili kukabili tatizo la ajira kwa vijana,
uamsikini, ujenzi wa uzalendo, maadili na mshikamano ndani ya jamii na
watanzania wanarukwa).
Hata
hivyo mwaka huu tayari tumekutana na kuzungumza na mkuu wa wilaya ya
sumbawangana Mh Sedoyeka na mkuu mpya wa mkoa wa Rukwa, Mh Mgalula Sai Mgalula ofisini kwake tarehe
30/09/2015 mambo mbalimbali pamoja na
umuhimu wa kuwawezesha wananchi ndani ya mkoa kupata Elimu juu ya umilikaji wa
ardhi/mashambayao kupimwa na wapate hati miliki ili kuongeza thamani ya ardhi,
kupunguza migogoro ya ardhi na kutumia ardhi kupata mitaji/kwa njia ya mikopo
kwenye vyombo vya fedha.
No comments:
Post a Comment
regnard