Ndugu wanajumaru leo jumatano Mwenyekiti Jumaru taifa Bi Helena Khamsi amefanikiwa kufanya kikao na mkuu wa mkoa wa Rukwa Ofisini kwake akiongozana na jopu la viongozi wa Jumaru Taifa ( wazee na sekretarieti) . Mara baada ya kumaliza kikao hicho Mama huyo amefanikiwa kutembelea maeneo ya chuo cha Kandala kilichofanyiwa ukarabati wa majengo kwa ajili ya kuanzisha chuo kikuu tawi la St Joseph Mkoa wa Rukwa. Mwisho mwenyekeiti alimalizia na vikao na viongozi wa matawi ya Jumaru katika ukumbi wa Betrehemu center na kupisha muda wa kuongea na Wakuu wa wilaya ya Kalambo, Nkasi na Sumbawanga hususani na Kijiji cha ajira ya ajira kwa vijana kinachotarajiwa kuanza katika mkoa huu chini ya JUMARU. Mbele ya mama khamsini viongozi wameeleza maendeleo ya matawi katka matawi yao na changamoto wanazokumbana nazo. Taarifa za nini kilijili katika ziara hii nitaendelea kukujuza kupitia hapa.
|
Mwenyekiti wa Jumaru Taifa (Kulia) akiwa na mkuu wa mkoa wa Rukwa (kushoto) ofisini kwa mkuu wa mkoa |
|
Viongozi wa Jumaru wakiwa katika jengo la walei Katandala na hilo nyuma yao ni jengo lililofanyiwa ukarabati tayari kwa kuanza chuo kikuu cha St Joseph. |
baadhi ya video na picha utazipata kwenye Group la JUMARU la whatsup kwa namba
0757230097
No comments:
Post a Comment
regnard