Kwa
namna ya kipekee kabisa JUMARU tunaomba tutumie fursa hii mbele ya watanzania wote kutoa pongezi na
shukrani maalumu kwa viongozi wetu wote ambao walipata nafasi ya kuutumikia
mkoa wa Rukwa wa zamani na baadaye mikoa ya Rukwa na Katavi ndani ya kipindi
cha 2000 – 2015, wa kuchaguliwa (yaani wabunge na madiwani wote) na wale wa
kuteuliwa na rais (yaani wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi
wa Halmashauri) na wakuu wa idara wote katika ngazi ya mkoa, Wilaya na
Halmashauri pamoja na watumishi wote kwa ujumla,kwa kuwezesha mikoa yetu
kuendelea kusonga mbele vyema katika
Nyanja zote za kimaendeleo na kiuchumi, kiutamaduni, kijamii na kisisasa.
Lengo langu la kutoa makala hii kwa wasomaji, kwa niaba ya jumuiya nzima ya wanarukwa na katavi ni kutaka kutoa pongezi
maalum kwa wabunge wetu wote na madiwani wao ambao wamekuwa wasimamizi na wahamasishaji
wakuu wa shughuli za maendeleo yetu. Hongeleni sana.
Hii ni kutokana na
ukweli kwamba katika kipindi hiki cha miaka 15
yaani 200 - 2015 mikoa yetu imepiga hatua kubwa za kimaendeleo katika
maeneo mengi ambayo huko nyuma hayakutegemewa kufikia hatua tulipo sasa, hasa kwenye
miundombinu za barabara za lami na
hata za changarawe zinazo pitika wakati wote wa mwaka kuliko ilivyo kuwa awali,
nishati ya umeme hadi vijijini, huduma ya maji,kuongezeka kwa shule za msingi,sekondari
na vyuo, viwanda vya mazao,mwamko mkubwa wa dhana ya ujasiriamali ndani ya
jamii yetu,mitandao ya mawasiliano,
vyama vya kuweka na kukopa, kuongezeka kwa zahanati na vituo vya afya na
uboreshaji wa hospitali ya mkoa wa Rukwa na za Wilaya.
Pia tumeweza kupata
maeneo mapya ya kiutawala katika kusogeza karibu huduma za kijamii kwa wananchi
hasa kuundwa kata mpya, tarafa, Wilaya, Halmashauri na mkoa. Hizi zote ni
jitihada kubwa zilzofanywa na viongozi wetu hawa wa mwaka 2000-2015.
Mwaka 2000 tulikuwa na
mkoa mmoja, Wilaya tatu na halamsahauri tano na leo tunazungumzia mikoa miwili, Wilaya sita na halamsahauri
tisa, awali hatukua na manispaa hata moja na sasa tuna manispaa mbili (Manispaa ya Sumbawanga
na Manispa ya Mpanda). Na pia kuna baadhi ya vijiji amavyo ni makao makuu ya
tarafa vimepandishwa hadhi na kuwa miji midogo na makao makuu ya kila Wilaya
yamepewa hadhi ya miji. Haya yote ni maendeleo na viashiria vyake.
Kusukuma
maendeleo ya kweli kunahitaji kujitolea kwa dhati na kujitoa mhanga.Kwa maendeleo
haya machache tuliyoyataja na mengi ambayo hatutayataja kutokana na urefu wa
orodha, yamewezekana na kuchangizwa kwa sehemu kubwa na nafasi na uzalendo wa ndugu
yetu mpendwa mzee Mizengo Kayanza Peter Pinda hasa akiwa mbunge na waziri wa
TAMISEMI na kisha akawa waziri mkuu wa Tanzania. Kwa uthubutu wake tuna mambo
mahususi ambayo tuna kila sababu ya kutambua mchango wake binafsi na
uunganishaji wake wa wabunge wa mikoa yetu uliotukuka na kumpa pongezi maalum.
Baadhi ya mambo hayo machache ni kama: -
1.
Kusukuma na kutunisha mfuko wa Elimu
mkoa wa Rukwa kwa kumbukumbu ya hayati Mwl. J. K. Nyerere ambao ulibuniwa mwaka
1999 na kuanza kutekeleza malengo yake
mwaka 2006 na mpaka unakabidhiwa rasmi kwa mkuu wa mkoa wa Rukwa mwaka
2010 ulikuwa umesaidia kupunguza tatizo la uhaba wa walimu kwa kuleta na kutoa
motisha kwa walimu zaidi ya 800 wa diploma, Digrii na Crush programme kwaajili
ya sekondari na chuo cha ualimu Sumbawanga, kusaidia kuanzisha shule sita za O’level
(shule za sekondari Kalambo, Muze, Katuma, Rungwa, Ilemba na Usevya) na shule
za A’level (Matai, Mambwe, Kizwite, Nkasi, Kate, Sumbawanga, Usevya na ) ambazo
zisingeanza bila mfuko kudhamini wizarani kwa mfuko kubeba jukumu la kutafuta walimu hitajika na
wabunge wamajimbo husika kuchukua jukumu la kushawishi na kushrikiana na halamsahauri
zao katika kujenga miundombinu hitajika na vifaa.
Mzee
Pinda aliwezesha mfuko huo kufanya harambee kubwa hapa Dare s salaam chini ya
ugeni rasmi wa Rais wa awamu ya nne.mh. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na kupata
fedha zilizo saidia kuendelea kutafuta manesi, walimu na madaktari kwa ajili ya
huduma ya afya na fedha zilizobaki ziliweza kutumika kuchangia ujenzi wa
madarasa na hosteli za wasichana kwenye baadhi ya shule na nyingi zaidi ya
milioni 250 zilinunua hisa/vipande kwenye mfuko wa umoja (UTT) na kwenye benki
ya CRDB ili faida itakayo kuwa inapatikana itumike kusomesha watoto yatima na
kudhamini watumishi kujiendeleza kitaaluma.Pia aliwezesha kupatikana mradi wa
chuo cha VETA Mpanda.
Ndugu wanarukwa na wanakatavi
Jitihada za mfuko huu zimewezesha kuutangaza
vema mkoa wa Rukwa kwa wakati huo,kupanda kwa kiwango cha ufaulu, ongezeko la
shule za kidato cha nne na cha sita. Miongoni mwa shule za kidato cha sita kati
ya zilizoanzishwa kwa jitihada za mfuko iliweza kutoa mwanafunzi aliyefaulu vizuri
na kuongoza kitaifa na shule yenyewe kushika nafasi nzuri kitaifa.
Kwa
kuwa ni wazi kwamba ili wanadamu wamjue Mungu ni lazima wawe na Elimu ya
kutosha, na kwakuwa mzee Pinda amesaidia jamii ya wanarukwa na Katavi kupata
Elimu, hivyo basi mzee huyu tayari amepata thawabu kwa Mwenyezi Mungu maana
amesaidia watu wake wamjue na kumtambua kupitia maandiko na upeo na uelewa
waliopata.
2.
Jambo
la pili kubwa alilofanya kwa uthubutu wake ni la
kuanzisha mkoa mpya wa Katavi ambalo limeongeza na kusogeza fursa nyingi za
kimaendeleo.Sasa tuna maeneo mengi mapya ya kiutawala ambayo yamesogeza karibu
huduma za kiuchumi na kijamii na kuongeza nafasi na fursa za ajira kwa makundi
mengi na kada mbali mbali kwenye mfumo rasmi na usio rasmi – maana miradi mingi
imebuniwa na kuleta fedha.
3.
Jambo
la tatu – ni kusukuma na kukamilika kwa Mradi wa miaka mingi
wa barabara ya lami Sumbawanga – Tunduma na jitihada zake za kutafuta na
kufanikisha Mradi wa barabara za lami za
Sumbawnaga- Mpanda na Sumbawanga – matai
- Kasanga na Matai-Kasesya japo hazijakamilika lakini walau kuna sehemu
kubwa za kuonekana. Pia kuna barabara nyingi za changarawe zimepasuliwa na
zingine kuboreshwa kwa viwango imara sana pamoja na madaraja muhimu. Kuna
vijiji toka uhuru havikuwahi kuona “bus” hata kidogo(Kala na Wampembe) lakini
hivi sasa wamesahau kabisa historia hiyo kutokana na uwingi wa vyombo vya
usafiri vinavyo wafikia kutokana na uzuri wa barabara zilizi chongwa na
kuwekewa utaratibu mzuri wa ukarabati.
Hii
ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa uwanja wa ndege Mpanda na Sumbawanga.Hongera
sana mzee Pinda.
4.
Jambo
la nne-ameweza kusukuma miradi ya umeme kwenye eneo letu
na kuwezesha baadhi ya maeneo yaanze kupata nishati husika na kusahau adha za
huko nyuma.
5.
Jambo
la tano-aliweka msukumo
mpya mkubwa kwenye kilimo na matumizi ya powertiller na ufugaji wa nyuki,
miradi ambayo imebeba taswira yake binafsi akiwa waziri mkuu, uzalishaji wa
mazao umepanda sana ukilinganisha na huko nyuma.
Aidha
naomba katamka kwamba mzee huyu
amesaidia sana mambo mengi(orodha ni ndefu sana) kupata msukumo wa utekelezaji
ndani ya eneo letu la Rukwa na Katavi.Itoshe tu kufahamika kwamba hakuna binadamu anayeweza
yote na tena peke yake,na mkamilifu ni Mungu peke yake. Hivyo basi tunaomba
kumpa pongezi maalum za dhati mzee wetu kwa utumishi wake wa kisiasa kwa
kipindi chote na kustaafu salama nafasi ya uwaziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Uwaziri
mkuu wake umetupatia sifa na heshima kubwa sana ndani na nje ya nchi, pale inapotafutwa
Mh. Pinda anatoka wapi.
Naomba kumaliza kwa kusema, mkuu wa
wanasayansi na anga akiwa na wasaidizi
wake angani (astronomers)
aliwaambia,”tambueni ya kwamba asiyejua aendako
hawezi kupotea njia”.
“Viva
mzee mizengo Pinda”
Ahsante sana.
Ndugu wasomaji,,kwa
heshima na taadhima tunaomba,kwa niaba ya jumuiya hii upatapo ujumbe huu mfikishie mzee
Pinda hiki tulichomwandalia kwa ishara ya kutambua utumishi wake kwetu wana
Rukwa na Katavi .